12 Novemba 2018

12 Novemba 2018

Jaridani hii leo mwenyeji wako ni Flora Nducha ambapo anaanza kwa kuangazia suala la usugu wa viuavijasumu kwa vijiumbe maradhi na kampeni ya wiki nzima iliyoanza hii leo ili kuelimisha umma juu ya dawa hizo ambazo hutumika kwa wanyama na binadamu. Anabisha hodi nchini Chad ambako Umoja wa Mataifa umeleta matumaini tena kwa wakulima wa zao la ufuta ambalo ni zao tegemewa kwenye nchi hiyo iliyoko ukanda wa Sahel. Mabadiliko ya tabianchi yalileta kilio lakini sasa wakulima wanacheka na wanafurahia maisha. Kisiwa pia cha Goree huko Senegal nacho kinamulikwa hii leo ambako mradi wa Benki ya Dunia umesababisha wananchi sasa kuweza kuona nuru kwenye maisha yao kwani jenereta za umeme ambazo umeme wake haukuwa wa uhakika zilikuwa zinaleta kilio mara kwa mara. Je nini kimefanyika? Ungana nasi bila kusahau makala ambayo leo inamulika ibara ya Nane ya Tamko la haki za binadamu kuhusu haki ya mtu kupata msaada wa kisheria na mchambuzi ni Robi Chacha kutoka Kenya. Usisahau mashinani leo tunabisha hodi Tanzania kuangazia kampeni moja ya TAMWA. Karibu!

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
12'57"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud