Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

9 Novemba 2018

9 Novemba 2018

Pakua

Jaridani hii leo Siraj Kalyango anaanzia huko Yemen ambako mashirika ya Umoja wa Mataifa bado yanapaza sauti ya kwamba machafuko  yanayoendelea huko Hudaydah yanakwamisha harakati za usambazaji wa misaada. Anabisha hodi pia ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati kunakoelezwa kuwa angalau usaidizi uliopatikana utawezesha wanafunzi kusoma muhula mzima wa masomo hadi mwaka 2019. UN News imezungumza na Matthias Schmale ambaye ni mkuu wa operesheni za UNRWA mjini Gaza. Muasi mzee zaidi duniani anaangaziwa leo ambaye si mwingine bali mzee Harry Smith kutoka Uingereza, yeye alipigana Vita Kuu ya pili ya dunia na anasimulia kwa hisia kali alivyosaidia wakimbizi bila kujali walikotoka. Makala leo ni Ibara ya 7 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa na mchambuzi wetu ni mwanasheria Fatma Karume kutoka Tanzania. Neno la Wiki leo kutoka BAKIZA, mchambuzi Bi. Mwahija Ally Juma anafafanua  maneno Sahihi na Saini!  Karibu!

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
12'