Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa kusaidia manusura wa utesaji waleta nuru kwa jamii

Mfuko wa kusaidia manusura wa utesaji waleta nuru kwa jamii

Pakua

Ibara ya 5 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwaka huu wa 2018, inaweka bayana kuwa hakuna mtu yeyote anayepaswa kuteswa kwa sababu yoyote ile. Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimetia saini na kuridhia tamko hilo lakini bado baadhi zinatuhumiwa kutesa watu kwa sababu mbalimbali jambo linaloleta ulemavu, madhara ya kisaikolojia na hata wengine hujiua. Je ni kwa kiasi gani madhila hayo yanakumba watu? Na huwa wanajisikia vipi wakati wa mateso na hata baada ya mateso? Jamii zao je? Basi  ungana na Assumpta  Massoi kwenye makala hii iliyowezeshwa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR.

Soundcloud
Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
3'33"
Photo Credit
UN Photo - Jean-Marc Ferre