Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akibutubia WebSummit Ureno, Guterres ataka silaha zenye uwezo wa kuua binadamu kwa kulenga na kujifyatua, zipigwe marufuku

Akibutubia WebSummit Ureno, Guterres ataka silaha zenye uwezo wa kuua binadamu kwa kulenga na kujifyatua, zipigwe marufuku

Pakua

Maendeleo ya teknolojia za kisasa yana faida na hasara zake kwa maisha ya binadamu hivi sasa kwa hiyo ni lazima kuchukua hatua ili kuhakikisha faida inakuwa kuwa kubwa kuliko hasara.

Amesema hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia jukwaa la wavuti linalofanyika huko Lisbon, Ureno ambapo amesema licha kwamba teknoloja hizo zinarahisisha kazi kama vile utambulisho wa binadamu , kusambaza mgao wa fedha na hata kubaini maeneo yaliyopimwa bado nyingine zinapaswa kuangaliwa upya.

Bwana Guterres ametolea mfano wa akili bandia ambayo inatumika hivi sasa na hata kuwezesha baadhi ya makombora kuweza kuamua eneo ambako linatakiwa kulengwa na hatimaye kufyatuliwa.

Katibu Mkuu amesema “mashine ambazo zina uwezo na utashi wa kuua binadamu hazikubaliki kisiasa, zinachukiza kimaadili na lazima zipigwe marufuku kwa mujibu wa sheria za kimataifa," akisema kuwa kadri akili bandia inavyoingizwa katika masuala ya silaha zinazojiendesha zenyewe na kuchagua eneo la kulenga, itakuwa vigumu kuepukana na kupanua kwa mizozo na kuhakikisha kuwa sheria za kimataifa za kibinadamu na zile za haki za binadamu zinazingatiwa.

Katibu Mkuu amesema hilo ni moja  ya mambo ambayo anaona ni changamoto za kasi ya ukuaji wa teknolojia za hali ya juu.

 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Arnold Kayanda
Sauti
2'44"
Photo Credit
UNMISS/Ilya Medvedev