Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu ya kifo sio dawa ya uhalifu- Bwana Ouko

Hukumu ya kifo sio dawa ya uhalifu- Bwana Ouko

Pakua

Ibara ya tatu ya  haki za bindamu inasema kuwa kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya kuwa huru na kulindwa. Lakini  mara nyingine haki hii hukiukwa kwa sababu mbali mbali.

Na endapo hukumu ya kifo ikitekelezwa basi husababisha mtu kunyimwa haki hii iliyoorodheshwa katika tamko la haki za binadamu.

Peter Ouko alihukumiwa kifo kwa sababu ya uhalifu na akaponea chupuchupu kwa msamaha wa rais. Sasa anafanya kazi yakuelimisha na kuwashauri vijana kutoshiriki uhalifu kupitia shirika la kirai, crime si poa ikimaanisha uhalifu sio jambo nzuri. Bwana Ouko amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii na kumuelezea safari yake gerezani na hisia zake kuhusu hukumu ya kifo.

Soundcloud
Audio Credit
Anold Kayanda/ Grace Kaneiya/ Peter Ouko
Audio Duration
3'46"
Photo Credit
UN Photo.