Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania bado kuna changamoto ya utekelezaji wa haki za binadamu

Tanzania bado kuna changamoto ya utekelezaji wa haki za binadamu

Pakua

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi disemba mwaka huu wa 2018 linatimiza miaka 70. Tamko hilo ni msingi wa haki za binadamu ulimwenguni kote na lilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Kuelekea maadhimisho hayo leo tunaangazia Ibara ya kwanza ya tamko hilo lenye ibara 30 ambayo inasema“Watu wote wamezaliwa huru hadhi na haki zao ni sawa  wote wana akili  na wana dhamiri hivyo yapaswa watendeane kindugu” Lakini je ibara hii inatekelezwa ipasavyo? Flora Nducha anazungumza na Anna Henga mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania anayeanza kwa kufafanua   changamoto za utekelezaji nchini humo.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
UN Photo.