Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiwa na kiongozi mvumilivu utakula mbivu:Jane Kamau

Ukiwa na kiongozi mvumilivu utakula mbivu:Jane Kamau

Pakua

Kongamano la kimataifa la wanawake viongozi kutoka barani Afrika lilokuwa linafanyika mjini Bujumbura,Burundi limekunja jamvi kwa kuwahamasisha wanawake kujitokeza mstari wa mbele kuchangamkia  nyadhifa mbalimbali za uongozi nana mustakhbali wa mataifa yao. Hili ni moja ya malengo muhimu ya maendeleo endelevu SDG’s yanayochagiza mataifa kutoa fursa na kuwawezesha wanawake kama usawa wa kijinsia unaojumuisha kushika nafasi mbalimbali za maamuzi ifikapo mwaka 2030.

  Katika kongamano hilo liloongozwa na Mkewe Rais wa Burundi Denise NKURUNZIZA,  limewaleta pamoja wanawake viongozi kutoka nchi za Maziwa  makuu na  Afrika ya Mashariki. Ili kufahamu zaidi yaliyojiri na kujadiliwa mwandishi wetu waMaziwa Makuu Ramadhani KIBUGA akiwa mjini Bujumbura  amezungumza na Jane KAMAU kutoka Kenya mmoja wa washiri anayeaanza kwa kuelezea umuhimu wa kongamano hilo na lilivyowachagiza wanawake katika masuala ya uongozi.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Ramadhan Kibuga
Audio Duration
4'43"
Photo Credit
PICHA: UNHCR/Maktaba/Eduardo Soteras Jalil