Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa nishati ya kutosha unakwamisha biashara Kagera, Tanzania

Ukosefu wa nishati ya kutosha unakwamisha biashara Kagera, Tanzania

Pakua

Upatikanaji wa nishati ni muhimu kwa ajili ya kuwezesha biashara na maisha kwa jamii ikiwemo kwa wakazi wa mkoa wa Kagera nchini Tanzania ambao wanaendesha biashara mbali mbali kwa ajili ya kukimu mahitaji yao. Nishati jadidifu sio tu zinawaletea hasara za kiuchumi lakini pia za kiafya na pia kuhatarisha maisha ya mtumiaji. Mathalani matumizi  ya mshumaa, si endelevu na ndio maana Umoja wa Mataifa unataka serikali na wadau kusaka mbinu za kuwa na nishati bora na endelevu. Je wakazi wenyewe wa Kagera wanasemaje? Ungana basi na  Tumaini Anathory wa radio washirika Radio Karagwe FM, ya mkoani Kagera, Tanzania ambaye amevinjari na kupata maoni ya baadhi ya wakazi kuhusu changamoto za upatikanji wa nishati.

Soundcloud
Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
50"
Photo Credit
Jiko la mkaa lionalotoa hewa chafuzi.(Picha:UM/Sophia Paris)