Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunasonga mbele licha ya changamoto- UN

Tunasonga mbele licha ya changamoto- UN

Pakua

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ikiwa ambapo chombo hicho kilichoanzishwa miaka 73 kinaendelea na majukumu yake ya kusongesha amani, haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi na kijamii licha ya changamoto lukuki zinazokumba dunia. Siraj Kalyango na maelezo zaidi.

Katika ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema shida ni nyingi lakini hizo si vikwazo kwao kwa kuwa watendaji wa chombo hicho na mashirika yake, kutwa kucha wanaendelea kukwamua maisha ya wananchi ili kukidhi kauli ya Sisi Watu iliyomo kwenye mkataba ulioanzisha Umoja wa Mataifa mwaka 1945.

Mfano huko Tanzania Miradi inayotokelezwa na shirika la chakula na kilimo duniani FAO kwa lengo la kuongeza tija kwenye kilimo, imesaidia wakulima siyo tu kuondokana na njaa bali pia kuboresha lishe na kuinua kipato.

Mwakilishi mkazi wa FAO nchini humo Fred Kafeero akihojiwa na Stella Vuzo wa UNIC Tanzania ametolea mfano wa mradi wa kilimo kinachohimili tabianchi ambao unatekelezwa mkoani Kagera akisema, "Ni kwa kutambua kuwa tabianchi inabadilika kwa hivyo kubadili pia mbinu za kilimo ili wakulima nao waendeleze uzalishaji wao na wapate kipato. Kwa hivyo tuna mradi huo ambao unaendana na ainisho la kilimo ukijumuisha mazao, mifugo na uvuvi ambapo tunafanya kazi na wakulima wa vijijini, wanawake na vijana  na kuwawezesha kufanya maamuzi ya kile wanachotaka kupanda na wanataka kupanda vipi. Lakini pia kuleta mfumo wa mashamba darasa ambako wanaweza kujifunza na kubadilisha ujuzi miongoni mwao.”

 

Mkoani Kigoma nako ambako wimbi la wakimbizi linaleta changamoto kubwa, mradi wa FAO wa kilimo bora kinachohimili tabianchi kimemnufaisha Lucy Lugano, mwakilishi wa kikundi cha wakulima walipokea mafunzo ya awali kutoka FAO.

Audio Credit
Flora Nducha/Siraj Kalyango
Audio Duration
2'31"
Photo Credit
FAO/Alessandro Stelzer