Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sote tuwe wainjilisti wa dunia yenye mazingira bora- Rocky

Sote tuwe wainjilisti wa dunia yenye mazingira bora- Rocky

Pakua

Nyota ya mwanamuziki mashuhuru kutoka Ghana, Rocky Dawuni inazidi kung'ara  katika anga za kuchechemu dunia kutekeleza yale yaliyo bora kwa maslahi ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Mwanamuzi huyu ambaye amekuwa akitumia kipaji chake cha kuimba kupazia sauti masuala yanayoweka hatarini mustakabali wa binadamu, amezidi kuonekana na hata kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa taasisi mbali mbali ikiwemo zile za Umoja wa Mataifa. Katika makala hii, Assumpta Massoi anaangazia kile ambacho amekipata Rocky Dawuni hivi karibuni, hatua ambayo ni kichocheo kwa wengine kama yeye kufuata hatua zake.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
2'47"
Photo Credit
(Picha: Idhaa ya Kiswahili/Grace Kaneiya)