Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukifanikiwa katika kilimo na utalii, tutafanikisha SDGs Msumbiji:Rais Nyusi

Tukifanikiwa katika kilimo na utalii, tutafanikisha SDGs Msumbiji:Rais Nyusi

Pakua

Mchakato wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s hautaki papara bali unahitaji busara na kutoa kipaumbele katika malengo mama. Hayo ameyasema Rais wa Msumbiji Fillipe Nyusi alipozungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili wakati wa mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 unaoendelea mjini New York Marekani.

Rais Nyusi amesema malengo 17 ni mengi na kuweza kuyafanyia kazi kwa wakati mmoja ni mtihani mgumu, ila kwa kutoa kipaumbele kwanza kwa  malengo yanayoonekana kuwa ndio muhimili wa mengine italisaidia taifa hilo la kusini mwa Afrika kufanikisha ajeda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 ya malengo hayo.

 Katika makala hii Rais Nyusi anaanza kwa kufafanua ni malengo yapi waliyoyapa kipaumbele cha kwanza.

Soundcloud
Audio Credit
Siraj Kalyango/Flora Nducha
Audio Duration
4'17"
Photo Credit
Daniela Gross