Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa TB si kulogwa, muhimu ufuate masharti ya matibabu -DJ Choka.

Ugonjwa wa TB si kulogwa, muhimu ufuate masharti ya matibabu -DJ Choka.

Pakua

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani WHO iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuwa ugonjwa wa Kifua Kikuu  ndio unaongoza kwa kuwa ugonjwa hatari zaidi wa kuambukiza duniani. Takwimu za hivi karibuni zaidi za Umoja wa Mataifa zinasema kuwa hivi sasa watu milioni 10.4 duniani kote wameambukizwa ugonjwa huo huku milioni 1.6 wakifariki dunia kila mwaka. Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la afya .WHO linataka mbinu mtambuka za kuondokana na ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030. Miongoni mwa mbinu hizo ni kutumia manusura wa ugonjwa huo kama wajumbe wa kuelimisha jamii ili ijikinge au isake tiba. Nchini Tanzania, mmoja wa manusura wa TB, Hugoline Martine almaarufu DJ Choka ameamua kufuatia mkondo huo wa kuelimisha jamii kuhusiana na ugonjwa huo na ili kufahamu kile anachofanya, Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungmza na DJ Choka na anaanza kwa kuelezea safari yake hadi kubaini ana TB.

Soundcloud
Audio Credit
Siraj kalyango/Anold Kayanda
Audio Duration
3'27"
Photo Credit
Tiba dhidi ya Kifua Kikuu huhusisha matumizi ya mchanganyiko wa dawa. Picha: UM