Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wimbo, ‘usichezee maisha yako’ watahadharisha vijana wanaofanya safari hatarishi

Wimbo, ‘usichezee maisha yako’ watahadharisha vijana wanaofanya safari hatarishi

Pakua

Kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine au hata nchi moja hadi nyingine ni haki ya kila mtu ali mradi anatimiza masharti ya nchi anakoelekea. Hata hivyo  uhamiaji unaohusisha usafirishaji haramu unahatarisha maisha ya wengi na kulifanya jambo la uhamiaji ambalo limekuwepo tangu jadi kuonekana kama kitu kibaya.

Dunia imeshuhudia maelfu ya watu wakihama wakiwemo vijana kuvuka baharí kutafuta fursa bora wakilinganisha na mazingira wanakotoka. Lakini safari hizi mara nyingi huishia pabaya huku watu wakipoteza hata maisha, ni kwa mantiki hiyo ambapo wanamuziki kutoka Afrika Magharibi moja ya eneo ambako hususan vijana wanatokea wakitafuta maisha bora bara Ulaya wametunga wimbo ukitoa tahadhari kwa wahamiaji. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala ifuatayo kufahamu ujumbe wao.

 

Audio Credit
Siraj Kalyango/Grace Kaneiya
Audio Duration
4'39"
Photo Credit
Photo: UNHCR/Iason Foounten