Wanawake Burundi wapata mwamko kujiendeleza kiuchumi
Pakua
Huko Burundi, wanawake wameanza kuchangamkia biashara ndogondogo ili kustaawisha familia zao.Takwimu zinaonyesha kuwa asimilia 53 ya raia wa nchi hiyo ya Burundi ni wanawake, lakini bado changamto kubwa ni umaskini unaowazingira sehemu kubwa ya wanawake hao pamoja na shida za kiuchumi.
Lakini kuna nuru gizani kwani wanawake hao sasa wameanza kugundua kwamba kusubiri kushikwa mkono sio rahisi. Na ni bora kufikiria wenyewe kwanza chanzo cha kujiendeleza na kustaawisha familia zao. Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga amezungumza na wanawake hao katika soko mojawapo mjini Bujumbura na kupokea hisia zao ambapo Siraj Kalyango anasimulia katika makala ifuatayo.
Audio Credit
Grace Kaneiya/Siraj Kalyango
Audio Duration
4'14"