Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake nao wazidi kung’ara kwenye urushaji mateke

Wanawake nao wazidi kung’ara kwenye urushaji mateke

Pakua

Mara nyingi imekuwa vigumu sana kwa watu kuweza kuhusisha michezo na Umoja wa Mataifa wakidhani kuwa suala hilo halina nafasi kwenye chombo hicho chenye wanachama 193. Kutokana na fikra hizo mwaka 2001 Umoja wa Mataifa ulianzisha ofisi mahsusi ya michezo kwa ajili ya maendeleo na amani. Lengo ni kipigia chepuo suala la michezo ukisema ya kwamba michezo siyo tu inaleta pamoja watu mahasimu bali pia inaongeza kipato. Michezo hivi sasa tena hata ile ambayo awali ilionekana kuwa ni ya wanaume, sasa wanawake wameingia kwa kasi na kuweza kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi. Je ni kwa vipi? Ungana basi na Siraj Kalyango kwenye makala hii kuhusu Patricia Apolot, mwananasumbwi na mrusha mateke  kutoka Uganda.

Audio Credit
Anold Kayanda/Siraj Kalyango
Audio Duration
4'24"
Photo Credit
UN Photo.