Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki kimbilio kwa watoto wenye shida Afghanistan.

Muziki kimbilio kwa watoto wenye shida Afghanistan.

Pakua

Nchini Afghanistan, mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia umekuwa nuru kwa watoto na vijana hususan wanaotoka katika familia masikini. Mradi huo unatekelezwa katika taasisi ya taifa ya Muziki nchini Afghanistan, shule pekee ya muziki nchini humo ikiibua vipaji vya muziki miongoni mwa watoto kwa kuwapatia mafunzo mahsusi ya muziki sambamba na masomo ya kawaida. Watoto ambao kutwa kuchwa wanakumbwa na mizozo, hapa wanapata amani na hata kusahau kile wanachopitia. Je nini kinafanyika? Ungana basi na Assumpta Massoi anayekupeleka mjini Kabul.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
3'22"
Photo Credit
World Bank/Roxana Bravo