Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 Septemba 2018

14 Septemba 2018

Pakua

Ukosefu wa usawa wazidi kuweka pengo la ustawi wa wakazi wa dunia ya sasa. Huko Zimbabwe serikali  yafunga baadhi ya shule na maduka ya nyama kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa kipindupindu kwenye mji mkuu Harare. Nchini DR Congo nako Ebola yaripotiwa Butembo jimboni Kivu Kaskazini, makala leo inabisha  hodi Afghanistan ambako muziki waleta nuru kwa watoto hususan maskini na  neno la wiki leo ni Kobe, mchambuzi ni Onni Sigalla kutoka BAKITA, Tanzania, Karibu na mwenyeji wako ni Onni Sigalla.

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'2"