Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya batyaba hatarini kutoweka, Uganda

Lugha ya batyaba hatarini kutoweka, Uganda

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni, UNESCO linataja lugha kuwa hatarini kutoweka iwapo watoto hawatumii lugha hiyo kama lugha ya mama nyumbani mwao. Vipimo hivyo vya UNESCO vinapima idadi ya watu wanaozungumza lugha na umri wao ili kubainisha uhatari wa lugha kutoweka.

Nchini Uganda nchi ambayo inajivunia uwepo wa lugha mbali mbali inakabiliwa na hatari ya baadhi ya lugha kutoweka kufuatia kuhamahama kwa baadhi ya jamii ya makabila madogo. Moja ya lugha hizo ni ile ya watu wa jamii ya wabatyaba walioko magharibi mwa Uganda. Je hali halisi ikoje? Ungana na John Kibego ambaye amevinjari Hoima kwa undani wa makala hii.

 

Audio Credit
Siraj Kalyango/John Kibego
Audio Duration
3'46"
Photo Credit
UNESCO