Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya mchango wao maisha ya wanawake wengi bado ni duni.

Licha ya mchango wao maisha ya wanawake wengi bado ni duni.

Pakua

Kuna uhusiano kati ya mchango wa wanawake na mahitaji ya familia iwe ya kijamii au kitaifa. Inakadiriwa kuwa asilimia 41  ya familia ambazo zinaongozwa na wanawake ni maskini huku theluthi mbili ya wanawake duniani huishi katika nyumba zisizo na  hadhi. Tatizo lingine kwa wanawake linatajwa kama kutoweza kumiliki ardhi ambapo ripoti moja ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO ilionyesha kama wanawake wa vijijini ndio wanahusika na uzalishaji wa nusu ya chakula duniani. Licha ya mchango wao huo lakini bado maendeleo yao ni duni, je ni kwa nini na hali inakuwa vipi? Siraj Kalyango anazungumza na mmoja wao huko nchini Uganda.

Soundcloud
Audio Credit
Arnold Kayanda/Siraj Kalyango
Audio Duration
3'34"
Photo Credit
Wanawake nchini Uganda.(Picha:UNFPA)