Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Toka chupa za taka hadi mapambo ya ndani

Toka chupa za taka hadi mapambo ya ndani

Pakua

Jukwaa la kimataifa la uendelezaji wa biashara ya nje, WEDF limeanza leo huko Lusaka, mji mkuu wa Zambia likileta pamoja viongozi wa serikali na wafanyabiashara kwa lengo la kufungua milango ya biashara ya nje duniani.

Miongoni mwa washiriki ni Beatrice Nyatando, kutoka Zambia, mbunifu mitindo mbobezi ambaye amegeukia biashara ya kuokota chupa zilizotupwa ziwe za plastiki au za kupasuka na kuzigeuza mapambo.

Akihojiwa na Stella Vuzo wa Umoja wa Mataifa kando mwa jukwaa hilo, Bi. Nyantando ambaye sasa anauza chupa moja kwa dola tano amesema..

(Sauti ya Beatrice Nyantando)

“Nilijifunza. Nilikwenda kwenye intaneti na nikaona video ya jinsi ya kutengeneza hizi chupa nami nikaamua nijaribu. Na kuna msichana ambaye nafahamu anajua haya mambo niliendwa kwake na alinifundisha sana. Kila chupa inauzwa kwacha 50.”

Mjasiriamali huyo akaelezea matumaini yake kutokana na jukwaa hilo ambalo linatoa pia fursa ya kuonyesha bidhaa

(Sauti ya Beatrice Nyandando)

“Matarajio yangu ni kwa bidhaa zangu ziweze kuonyeshwa duniani kote ili angalau niweze kupata masoko hata nje ya Zambia.”

Jukwaa hili limeandaliwa na kituo cha biashara cha kimataifa, ITC, taasisi tanzu ya Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD ambapo taasisi hiyo imetumia fursa hiyo kuzindua SheTrades, mpango wake wa kusaidia wanawake kukuza na kuuza bidhaa zao nje ya mipaka ya nchi zao.

Audio Credit
Sharifa Kato
Sauti
1'20"
Photo Credit
UN Photo/Martine Perret