Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo chaleta nuru kwa wakazi kaunti ya Meru, Kenya

Kilimo chaleta nuru kwa wakazi kaunti ya Meru, Kenya

Pakua

Kilimo ndio uti wa mgongo ni usemi wenye maana kubwa sio tu kwa uchumi wa mataifa mengi yanayoendelea lakini pia kwa raia wa kawaida, na kwa mujibu wa shirikala Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, kilimo endelevu na chenye ufanisi zaidi ni kile kinachojali mazingira.

 Sasa shirika hilo limeamua kuanzishamafunzo maalumu kwa wakulima katika nchi nane duniani ili kuwapa mbinu za kilimo bora ambachi mbali ya kuwaongezea tija kitawasaidia kuhifadhi mazingira kwa ajili yao na vizazi vijavyo.

 Miongoni wakulima waliobahatika kupata mafunzo hayo ni wanawake wa kundi la Ithondio  katika County ya Meru nchini Kenya. Katika Makala hii Siraj Kalyango amefuatilia ufanisi na mafanikio yao baada ya mafunzo ya FAO, ungana naye

 

Soundcloud
Audio Credit
UN News/Siraj Kalyango
Audio Duration
4'37"
Photo Credit
Benki ya Dunia/Flore de Preneuf