Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yazindua kampeni ya chanjo dhidi ya kipindupindu-WHO

Uganda yazindua kampeni ya chanjo dhidi ya kipindupindu-WHO

Pakua

Kila mwaka nchini Uganda hutokea wastan wa visa1,850 vya kipindupindu na takriban vifo 45. Hii ni kwa mujibu wa waziri wa Afya wa Uganda Dkt Jane Ruth Acieng alipozungumza wakati wauzinduzi wa kampeni hiyo.

Visa vingi hutokea sehemu za Mashariki, kaskazini na kaskzini maghari mwa Uganda. Zoezi hili linadhaminiwa na  shirika la kimataifa la muungano wa chanjo ,GAVI na dawa inayotumika ya matone ndio inatumika kwa mara ya kwanza nchini Uganda.

Siraj Kalyango wa Idhaa hii amezungumza na waziri wa afya anehusika na shughuli za jumla , Dkt Sarah Opendi, kuhusu chanjo hii.

Audio Credit
Sarah Opendi
Audio Duration
2'41"