Demistura asema katiba ndiyo itaweka mambo sawa Syria

4 Septemba 2018

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya  Syria, Staffan de Mistura, amesema anatarajia kukutana na maafisa wa ngazi ya juu wa Urusi, Uturuki na Iran mnamo Septemba 10 na 11 , katika majadiliano ya muendelezo wa mikutano iliyofanyika Geneva na Sochi hapo awali.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva Uswisi,  de Mistura amesema kuunda kamati ya kusimamia mabadiliko ya katiba Syria ndio mtihani.

Audio Credit:
Grace Kaneiya
Audio Duration:
2'5"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud