Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa nimeelewa tamko la haki za binadamu ni sawa na sheria mama- Kijana kutoka Tanzania

Sasa nimeelewa tamko la haki za binadamu ni sawa na sheria mama- Kijana kutoka Tanzania

Pakua

Umoja wa Mataifa unaendelea kutumia kila mbinu huko mashinani kuhakikisha misingi na malengo yake vinafahamika vyema miongoni mwa siyo tu mamlaka bali pia wananchi. Mathalani tamko la haki za binadamu ambalo lilipitishwa takribani miaka 70 iliyopita, ndio msingi wa haki kuu za msingi za binadamu ambazo kwingineko zinaheshimiwa ilhali kwingine zinasiginwa.

Ni kwa kufahahamu hali hiyo ndio maana kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kiliendesha mafunzo ya vijana wanaohusika na sanaa zinazoonekana ikiwemo wachora vibonzo, katuni na graffiti. Vijana hao wanatoka shirika la kiraia la Mulika Tanzania linalohusika na masuala ya afya ya uzazi, elimu ya uraia na haki za binadamu kwa vijana. Stella Vuzo, afisa wa UNIC Dar es salaam, baada ya mafunzo hayo alipata fursa ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Mulika Tanzania, Hussein Mlele na mwanafunzi anayefanya kazi kwa vitendo na shirika hilo Catherine Joseph Madebe. Catherine anaanza kwa kuelezea alichojifunza.

 

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/Stella Vuzo
Audio Duration
4'29"
Photo Credit
Nchini Tanzania harakati zinaendelea ili kuwezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijasiriamali na hivyo kujinasua kutoka katika lindi la umaskini. (Picha:Benki ya Dunia-Tanzania)