Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sote tuwajibike na wakimbizi wa Rohingya:Guterres

Sote tuwajibike na wakimbizi wa Rohingya:Guterres

Pakua

Mzingo wa zahma ya wakimbizi wa Rohingya sio jukumu la serikali ya Bangladesh pekee bali unapaswa kuwa ni jukumu la dunia nzima. Wito huo umetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye kikao cha Baraza la Usalama kuhusu hali ya wakimbizi wa Rohingya, kilichofanyika kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Guterres amesema zahma hiyo iliyoanza mwaka mmoja uliopita jimboni Rakhine nchini Myanmar sasa imekuwa moja ya majanga makubwa kabisa ya kibinadamu na haki za binadamu duniani.

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
3'37"
Photo Credit
UN / Evan Schneider