Nishati ya kupikia bado ni mtihani mkubwa kwa wanawake Ziwa Albert

28 Agosti 2018

Upatikanaji wa nishati ya kupikia ambayo ni moja ya mahitaji ya msingi bado unakabiliwa na changamoto wakati huu ambapo kuna mwamko kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira na kutumia nishati mbadala.  

Mila na desturi katika jamii pia zinaonekana kuchangia katika kuongeza shinikizo zinazokabili wanawake katika kusaka kuni hususan maeneo ya vijijini ambako upatikanaji wa nishati mbadala ni ngumu.

Kwa wakaazi wa Ziwa Albert nchini Uganda, shughuli za kusaka kuni ni jukumu la wanawake pekee na wakati mwingine wanahofia usalama wakienda kusenya kuni hususan maeneo ya msituni. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amevunjari eneo hilo na kukutana na wanawake wakiwa katika harakati za kusaka kuni na kuzungumza nao katika Makala hii. Ungana naye.

Audio Credit:
Grace Kaneiya/John Kibego
Audio Duration:
3'50"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud