Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNIC Tanzania yanoa wachora vibonzo ili waeneze haki za binadamu

UNIC Tanzania yanoa wachora vibonzo ili waeneze haki za binadamu

Pakua

Suala la haki za binadamu ni moja ya misingi ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mwaka 1945. Na ndio maana chombo hicho kilipitisha tamko la haki za binadamu lililo msingi wa katiba, kwa nchi zilizoridhia nyaraka hiyo ikiwemo zile za Afrika Mashariki. Hivi sasa kuelekea miaka 70 ya tamko hilo, Umoja wa Mataifa unatumia kila mbinu kueneza haki hizo na hasa inatumia vijana kuhakikisha kupitia stadi zao wanaelimisha jamii juu ya haki kama za kuishi, kujieleza, kula, kucheza, kutembea na kadha wa kadha. Ni kwa mantiki hiyo kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC nchini Tanzania kilichukua jukumu la kuelimisha wasanii wakiwemo wachora vibonzo. Je nini wamefanya? Na je wamenufaika vipi? Stella Vuzo, Afisa Habari wa UNIC Dar es salaam amezungumza nao baada ya mafunzo.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Stella Vuzo
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
Picha:UNICTz/Stella Vuzo