Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 Agosti 2018

20 Agosti 2018

Pakua

Hii leo Patrick Newman anaangazia jinsi gani wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanamkumbuka Kofi Annan, KatibuMkuu wa 7 aliyefariki dunia jumamosi huko Uswisi. Naye Dkt. Salim Ahmed Salim, mwanadiplomasia kutoka Tanzania ambaye aliwahi kufanya kazi na hayati Annan ajibu hoja ya wale wanaosema Kofi Annan alishindwa huko Rwanda.  Anabisha hodi Lebanon ambako watoto wa wakimbizi wa Syria sasa wana nafuu kubwa kwani sasa watasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Na katika makala leo ni huko Yemen, Umoja wa Mataifa wasaidia makazi bora kwa wakimbizi walio kwenye maeneo yenye joto na  baridi kali. Hatimaye mashinani anakwenda mkoani Songwe nchini Tanzania, wakulima sasa wanasema afadhali. Kulikoni? Karibu

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
11'38"