Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za watoto ni haki za binadamu lazima ziheshimiwe:UNICEF

Haki za watoto ni haki za binadamu lazima ziheshimiwe:UNICEF

Pakua

Haki za watoto ni haki za binadamu na zinapaswa kuheshimiwa na kutekelezwa katika kila ngazi kuanzia kwenye familia, jamii na hata serikali kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Hata hivyo shirika hilo linasema mara nyingi hazitekelezwi hususan suala la ukatili, kuwatelekeza, mimba za utotoni  na hata kutowapa elimu. Nchini Tanzania serikali imelivalia njuga suala hilo likitaka kila kijiji, wilaya na mkoa kuchukua hatua kuhakikisha haki hizo zinatambuliwa na kuzingatiwa kwa kushirikisha wadau wote katika jamii wakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali. Licha ya juhudi hizo bado safari ni ndefu kufikia malengo hayo. John Kabambala kutoka Radio washirika TanzaniaKidsTime FM ametembelea wilaya ya Mteke mkoani Njombe ambako pamoja na kuwepo kwa shirika la kupigania haki na sheria katika jamii ukatili kwa watoto ni changamoto, ungana naye katika Makala hii kufahamu zaidi jitihada zinazofanyika.

Audio Credit
Siraj Kalyango/John Kabambala
Audio Duration
4'47"
Photo Credit
UN News