14 Agosti 2018
Pakua
Katika jarida hii leo Assumpta Massoi anaangazia yafuatayo:
- Jamii ya kabila dogo huko nchini Libya, yafurushwa kutoka makazi yao ya muda, wanawake na wasichana watishiwa kubakwa, hivi sasa wengine wanaishi kwenye magari, UNHCR yapaza sauti.
- Sasa wakimbizi hawapaswi kuhofia tena iwapo hawafahamu lugha ya kigeni kule wanakohamia kwa kuwa wasomi wawili kutoka Chuo Kikuu kimoja nchini Marekani wamekuja na apu itendayo miujiza, wewe nawe waweza kujitolea kusaidia kwa kuwa mkalimani au mtafsiri.
- Jamii za asili ni lazima ziangaliwe kwa jicho la kipekee katika kupima na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, amesema Dkt. Elifuraha Laltaika kutoka Tanzania
- Na makala Patrick Newman amebisha hodi nchini Lesotho, wanawake huko hawataki mchezo katika kukabiliana na umaskini.
- Mashinani ni Tanzania, mradi wa UNICEF waleta kicheko kwa wazazi wa wanafunzi mkoani Mbeya, Karibu!
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'58"