Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Natimiza ndoto ya dada yangu - Kijana Sharifa

Natimiza ndoto ya dada yangu - Kijana Sharifa

Pakua

Ndoto! “Ndoto yangu ni kuwa nataka kufanikiwa na kuleta mabadiliko katika jamii yangu”. Hiyo ni kauli ya kijana Sharifa Kato ambaye anasema amezaliwa katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam nchini Tanzania.

Licha ya mazingira yake duni utotoni, lakini ndoto yake ya kubadili maisha yake na ya familia ilimuwezesha kufungua milango ambayo ilionekana kama ni kizuizi na kukatisha tamaa wengi ambapo sasa msichana Sharifa  ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu kilichoko jimbo la   California,  California State Polytechnic Pomona ambako anasomea shahada ya uzamili ya utawala wa umma.   Katika makala hii  Sharifa amezungumza na Grace Kaneiya ambapo anaanza kwa kuelezea safari yake kutoka wakati alipomaliza shule ya sekondari, ungana naye.

 

Audio Credit
Siraj Kalyango/Grace Kaneiya
Audio Duration
4'18"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi