Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

07 Agosti 2018

07 Agosti 2018

Pakua

Jaridani  hii leo Jumanne ya Agosti 7 mwaka 2018 mwenyeji wako ni Assumpta Massoi na habari alizokuandalia hii leo:

  1. Chanjo dhidi  ya Ebola kuanza kutolewa wiki hii huko jimbo la Kivu Kaskazini nchini DR Congo, serikali na wadau wake wamejipanga vyema kudhibiti mlipuko.
  2. Nchini Yemen mitutu ya bunduki na milio ya makombora havikatishi tamaa wahudumu wanaotoa chanjo dhidi ya kipindupindu nchini  humo.
  3. Huko Somalia, raia waliokuwa wamesaka hifadhi Yemen wameendelea kurejea nyumbani kwa msaada wa UNHCR.
  4. Katika makala Patrick Newman anatamatisha wiki ya unyonyeshaji kwa kuangazia Tanzania.
  5. Na katika mashinani pia tunaangazia pia unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama na mwenyeji wetu ni Neema Joshua. Karibu!
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
10'36"