Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa inakabiliwa na changamoto , Tanzania inajitahidi kulinda misitu

Ingawa inakabiliwa na changamoto , Tanzania inajitahidi kulinda misitu

Pakua

Misitu ni uhai na kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP ili misitu hiyo inufaishe jamii, basi kila mtu anajukumu la kuhakikisha inalindwa kwa ajili ya kizazi hiki na kizazi kijacho.

Nchini Tanzania wito umetolewa kutafuta njia mbadala ya matumizi ya kuni, kuelimisha jamii na mjumuisha kila mtu katika kampeni hiyo. Wito huo umetolewa na Profesa Irmeli Mustalahti mhadhiri wa masuala ya sayansi ya jamii na utafiti katika chuo kikuu cha Eastern nchini Finland.

Raia huyu wa Finland amefanya utafiti wa uhifadhi wa misitu kwa miaka mingi nchini Tanzania. Akizungumza na Flora Nduchakatika makala hii amemueleza alichobaini Tanzania na kwa nini aliamua kwenda nchini humo.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Flora Nducha
Audio Duration
3'20"
Photo Credit
Misitu.(Picha;World Bank/Curt Carnemark