Burudani ya muziki huleta pamoja jamii tofauti

3 Agosti 2018

Sanaa ya muziki hutumika kuburudisha , kuelimisha na pia kuleta jamii mbalimbali pamoja.

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO,  limekuwa mstari wa mbele kuziwezesha jamii mbalimbali duniani siyo tu kukuza tamaduni zao kupitia sanaa ya muziki na hata sanaa ya maigizo bali pia kujifunza tamaduni za wengine kupitia sanaa hizo ili hatimaye kuimarisha utangamano.

Nchini Uganda mwandishi wetu, John Kibego alipata fursa ya kuzungumza na mholanzi ambaye ametunga wimbo kwa lugha ya kienyeji ili kuchagiza umoja na utangamano katika jamii.

Je ana ujumbe upi katika kibao chake? Ungana nao katika makala hii upate undani zaidi.

 

Audio Credit:
Patrick Newman/ John Kibego
Audio Duration:
3'42"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud