Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 Agosti 2018

02 Agosti 2018

Pakua

Hii leo Alhamisi ya Agosti 2, 2018 Patrick Newman anaangazia yafuatayo:

  1. Kulipuka tena kwa ugonjwa wa Ebola huko DRC ambapo sasa ni kwenye jimbo la Kivu Kaskazini. Umoja wa Mataifa  umechukua hatua kudhibiti mlipuko kwenye eneo hilo linalogubikwa na mapigano.
  2. Zimbabwe purukushani za baada ya uchaguzi zikiendelea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesihi pande zote  nchini humo ikiwemo wanasiasa, wananchi na wagombea wa urais kujizuia na hatua ambazo zitaendelea kudororesha amani.
  3. Yaelezwa kuwa SDGs mafanikio yake yategemea utashi wa kisiasa, tumezungumza na Innocent Maloba wa WWF.
  4. Makala leo inabisha hodi Tanzania ambako vijana wenye ushawishi wamekutanishwa na viongozi wa UN nchini humo kuona ni jinsi gani watasaidia kutokomeza ukeketaji.
  5. Mashinani tunasalia Tanzania hususan mkoani Tanga ambako mama mmoja anazungumzia unyonyeshaji wa mtoto wakati huu ambapo wiki ya unyonyeshaji duniani imeingia siku ya pili. KARIBU!
Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
11'24"