Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japo inajitahidi, Tanzania bado ina kibarua cha kutimiza SDG’s: Assad

Japo inajitahidi, Tanzania bado ina kibarua cha kutimiza SDG’s: Assad

Pakua

Tanzania imepiga hatua katika utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGS, lakini inakabiliwa na changamoto lukuki ambazo zisiposhughulikiwa malengo hayo hayatotimia ipasavyo. Hayo yamesemwa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini humo (CAG) Profesa Musa Juma Assad, katika mahojiano maalumu na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini New york Marekani. Profesa Assad alikuwa akihudhuria mkutano wa kimataifa wa tathimini ya utekelezaji wa SDG’s na mchango wa ofis iza ukaguzi wa hesabu za serikali katika kufanikisha malengo hayo. Ameweleza Flora Nducha mengi waliyoafikiana na nini Tanzania inapaswa kufanya kufikia malengo. Lakini kwanza anakumbusha walichoafikiana kwenye kikao cha kwanza

Audio Credit
Flora Nducha/Prof Assad
Audio Duration
10'25"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi