Methali ya ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno sasa ni dhahiri huko Kenya

Methali ya ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno sasa ni dhahiri huko Kenya

Pakua

Umoja wa Mataifa unataka mbinu mbadala za kupata nishati hiyo ya kupikia na ndio  maana nchini Kenya shirika la kiraia la Bright Green Renewable Energy limeibuka na mbinu ya kuzalisha mkaa wa kupikia kwa kutumia takataka iwe za majumbani au mashambani. Je nini wanafanya? Assumpta Massoi wa idhaa hii amezungumza na Chebet Lesan, Afisa Mtendaji Mkuu na muasisi wa shirika hilo, wakati alipotembelea Umoja wa Mataifa kushiriki mkutano wa kutathmini malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Bi Lesan anaanza kwa kujitambulisha vyema zaidi.

Audio Credit
Flora Nducha/ Chebet Lesan
Sauti
6'11"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi