Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusipotunza mazingira, hayatatutunza- Maloba

Tusipotunza mazingira, hayatatutunza- Maloba

Pakua

Utunzaji wa mazingira ni suala ambalo linahitaji ushiriki wa kila mtu kwani 'tusipotunza mazingira, hayatatutunza.' Hayo yamesemwa na Innocent Maloba kutoka shirika la World Wide Fund kwa ajili ya mazingira linalofanya kazi katika takriban nchi mia moja kote duniani. 

Bwana Maloba kutoka Kenya amesema utunzaji wa mazingira haupaswi kuonekana kama jambo la serikali tu, au sekta binafsi kwani athari zake zinashuhudiwa na wote na zisipozingatiwa hata vizazi vijavyo vitakumbwa na mtihani mkubwa na utimizaji wa malengo ya maendeleo SDG’s ifikapo mwaka 2030 itakuwa changamoto kwani mazingira ndio shina la mambo yote.

Kwa undani zaidi unagana na Grace Kaneiya katika Makala hii akizungumza na bwana Muloba kwenye makaoa makuu ya Umoja wa Mataifa jijini, New York Marekani kuhusu mazingira na anaanza kwa kuelezea shirika hilo linafanya nini?

Audio Credit
Siraj Kalyango/ Grace Kaneiya/ Innocent Maloba
Audio Duration
4'34"
Photo Credit
Jiko la mkaa lionalotoa hewa chafuzi.(Picha:UM/Sophia Paris)