Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa chakula kutoka Korea Kusini kukomboa wakimbizi Uganda

Msaada wa chakula kutoka Korea Kusini kukomboa wakimbizi Uganda

Pakua

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), nchini Uganda limepokea kwa mikono miwili, msaada wa chakula kutoka kwa Serikali ya Korea Kusini kwa ajili ya kusaidia wakimbizi katika nchi hiyo. 

Mchango huo wa tani 5,000 za mchele umepokea na WFP leo, kwenye ghala lake la chakula kule Tororo Mashariki mwa Uganda.

Akipokea mchango huo Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP Uganda El-Khidir Daloum amesema, utaisaidia kushughulikia mahitaji ya chakula ya msingi kwa wakimbizi wapatao 420,000 katika makaazi saba ya wakimbizi katika mwezi mzima wa Agosti.

Mchele huu utanufaisha wakimbizi katika makaazi ya Nakivale, Kyangwali, Kyaka II, Oruchinga, Palabek, Imvepi na Rwamwanja ambao mara nyingi hutarajia msaada wa unga wa mahindi.

Bwana Daloum amefurahishwa na mchango huo ambao ameuelezea kuwa ni wa kwanza kabisa kutoka kwa serikali ya Korea Kusini katika historia ya shughuli za kibinadamu kwa wakimbizi nchini Uganda.

Balozi wa Korea Kusini nchini Uganda Mheshimiwa Kim You-churl, amesema mchango huo umetolea kwa moyo mkunjufu wa watu wa Korea Kusini kwa ajili ya wanaokimbia migogoro nchini Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC0, na nchini nyingine katika eno la Maziw aMakuu.

Mchango huo umekuja wakati mashirika yakuhudumia wakimbizi nchini Uganda yanakabiliwa na ukata wa ufadhili kutokana na mmiminiko wa wakimbizi usiotarajiwa mnamo mwaka huu.

 

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
1'6"
Photo Credit
Watoto wakimbizi Uganda. Picha: UM