Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

“Kamata weka ndani kwa kutotii amri halali!”

“Kamata weka ndani kwa kutotii amri halali!”

Pakua

Utoro mashuleni ni moja ya tishio kubwa la kutotimiza lengo namba nne la maendeleo endelevu lihusulo elimu kama hautodhibitiwa nchini Tanzania. Sasa serikali imeamua kulivalia njuga sula hilo kwa kampeni ya mkoa kwa mkoa na mkono wa sheria.

Kampeni hizo ni za kuihamasisha jamii kuelewa umuhimu wa elimu, kuwafikisha mahakamani wazazi wasiohimiza watoto kwenda shule au wanaowafanyisha kazi watoto badala ya kuwapeleka shule , lakini pia maandamano ya amani kama yaliyofanyika mkoani Tabora wiki hii na kuhususisha viongozi wa serikali, waalimu, wazazi na wahusika wakuu ambao ni wanafunzi.

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
2'
Photo Credit
Wanafunzi darasani nchini Tanzania. Picha: UNICEF Video capture