Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwa mwanamke ni changamoto, na ni changamoto zaidi kuwa mwanamke mwenye ulemavu

Kuwa mwanamke ni changamoto, na ni changamoto zaidi kuwa mwanamke mwenye ulemavu

Pakua

Unyanyapaa bado upo kati ya wanawake na wanaume walio na ulemavu katika masuala mbalimbali kwenye jamii ikiwemo katika ufikiaji wa huduma muhimu na za msingi.  Hiyo ni kauli ya Seneta Isaac Mwaura kutoka Kenya katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili.

Akihojiwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Seneta Mwaura ambaye ana ulemavu wa ngozi amesema mtazamo wa jamii kwa watu walio na ulemavu una tofauti kubwa katika misingi ya jinsia. 

Audio Credit
Grace Kaneiya
Audio Duration
2'15"
Photo Credit
UN Photo/Mark Garten)