Madhara ya mifuko ya plastiki ni gharama kubwa kwa wakaazi Bujumbura
Mifuko ya plastiki imekuwa kero kwani ina madhara makubwa siyo tu kiafya bali pia kimazingira. Imesababisha kuziba kwa mifereji ya majitaka na huko kwenye maji ikiathiri pia viumbe vya majini. Barani Afrika kuna nchi ambazo zimepitisha sheria kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki kwa mfano Kenya na Rwanda na nyingine zikiweka mikakati kufikia hilo.
Serikali ya Burundi nayo imeanzisha mchakato unaonuwia baadaye kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Kwa hatua ya kwanza maafisa wa serikali na watetezi wa mazingira wameanza kutoa mafunzo kuhusu madhara ya kimazingira ya kutumia mifuko hiyo ya plastiki.Lakini changamoto kubwa ni kukosekana kwa mbadala ili kuweza kuachana na mifuko hiyo. Je nini kinafanyika zaidi na wananchi wanasemaji? Basi tuungane na mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga ametuandalia makala haya akiwa mjini Bujumbura.