Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wa Afrika wapelekwa kampasi ya Ali Baba kujifunza biashara za kielektroniki

Vijana wa Afrika wapelekwa kampasi ya Ali Baba kujifunza biashara za kielektroniki

Pakua

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imezungumzia ushirikiano wake na kampuni ya Ali baba katika kuinua uwezo wa vijana wa Afrika kwenye kutumia majukwaa ya kieletroniki kuuza bidhaa zao.

Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi amezungumzia mradi huo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Amesema wamanzisha mradi huo na Jack Ma, kiongozi wa kampuni ya Ali Baba ambapo vijana kutoka Afrika wanakwenda jimboni Hangzhou kujifunza jinsi ya kujenga majukwaa ya biashara mtandaoni.

Dkt. Kituyi amesema majukwaa ya aina hiyo yanasaidia kupunguza gharama za matangazo.

Halikadhalika faida nyingine ni kwamba inawezesha wafanyabiashara kufikia masoko  ya kimataifa.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'1"
Photo Credit
Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi akihojiwa na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Idhaa ya Kiswahili/Flora Nducha)