Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubunifu wahitajika katika kilimo kwenda sanjari na mahitaji ya watu

Ubunifu wahitajika katika kilimo kwenda sanjari na mahitaji ya watu

Pakua

Wakati  idadi ya watu duniani ikizidi kuongezeka, juhudi zaidi za ubunifu zinahitajika haraka ili kuweza kuongeza kiwango cha uzalishaji katika kilimo, kuboresha utoaji na usambazaji ili kukabiliana na upungufu na uharibifu wa chakula. Na juhudi hizo zihakikishe kuwa wote wanaokabiliwa na upungufu wa chakula na utapiamlo, wanapata chakula chenye lishe ili kwenda sambamba na lengo namba mbili la maendele endelevu ambalo ni kukomesha njaa.

Katika mukhtadha huo taasisi ya kitaifa ya utafiti wa kilimo nchini Uganda ya Kawanda inafanya utafiti wa aina za maharage ambayo yanamea haraka hata katika mazingira magumu na yenye kuzalisha mbegu nyingi. Kwa mengi zaidi ungana na Siraj Kalyango katika makala yafuatayo.

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Siraj Kalyango
Audio Duration
3'58"
Photo Credit
Picha: UM/Video capture