Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hata kama mamangu amebakwa nina haki

Hata kama mamangu amebakwa nina haki

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono kwenye mizozo, Umoja wa Mataifa mwaka huu unataka watoto waliozaliwa kutokana na ukatili wa kingono vitani watendewe haki. Patrick Newman na ripoti kamili.

Umoja wa Mataifa unasema hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa mara nyingi watoto wanaozaliwa kutokana na vitendo vya  ubakaji wakati wa migogoro hukabiliwa na tatizo la utambulisho katika jamii.

Akizungumzia madhila hayo, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono vitani, Pramila Patten ambaye ametembelea hivi karibuni kambi za wakimbizi warohingya huko Bangladesh waliokumbwa na ubakaji. amesema..

 Sauti ya Pramila Patten

Wanaogopa kupuuzwa na jamii ya  kimataifa. Wanataka haki: huo ndio ujumbe nilioupata kutoka kwa wengi kwa siku moja niliyokuwepo kambini. Wanataka wahalifuwafikishwe mbele ya sheria, na wanaelewa sana kinachoendelea sasa, na walinipatia taarifa zote; ya kwamba mauaji ya kimbari yanaendelea dhidi ya watu wao na wanataka ulimwengu mzima ufahamu hivyo.

Bi. Patten akazungumzia msaada unaotolewa kwa wanawake wajawazito na watoto waliozaliwa kutokana na vitendo vya ubakaji katika migogoro ya kivita.

 Sauti ya Pramila Patten

Nadhani bado kuna kazi zaidi ya kufanya.. Lakini kinachofurahisha ni kwamba kwamba tatizo hilo  linashughulikiwa na UNICEF. Lakini nadhani kama mtoto aliyezaliwa kutokana na ubakaji ametelekezwa, au amewekwa katika taasisi, au anatunzwa na  jamii, nadhani unyanyapaa aliopitia utabaki palepale. Wasiwasi wangu pia unahusiana na usajili wa uzazi kwa sababu nadhani kuna masuala mapana ya utambulisho wa kijamii na utambulisho wa kisheria.

 

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
1'54"
Photo Credit
UNICEF/Brian Sokol