Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila nishati katika jamii maendeleo ni mtihani

Bila nishati katika jamii maendeleo ni mtihani

Pakua

Nishati ya umeme inasalia kuwa muhimu sana katika maendeleo na ukuaji wa uchumi duniani kote kutokana na inavyohitajika katika matumizi ya kila siku ya watu, uzalishaji viwandani, miundombinu ya usafiri na kadhalika. Lakini kwa nchi nyingi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa nishati hiyo  na kuwafanya wengi kugeukia nishati mbadala kama ile itokanayo na mionzi ya jua au sola kwa ajili ya matumizi ya kila siku na zaidi kwani gharama yake ni nafuu na inapatikana kwa urahisi.

Mwandishi wetu wa maziwa makuu, Ramadhani kibuga alipata fursa ya kutembelea kitongoji cha Gatumba mjini Bujumbura ambako kutokana na ukosefu wa umeme wakazi wa eneo hilo wamefuata nyayo na kugeukia nishati mbadala ya sola. Je wana lipi la kusema kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo kupata nishati hiyo? Basi ungana naye katika Makala hii kupata majibu.

Audio Credit
Siraj Kalyango/ Ramadhan Kibuga
Audio Duration
6'
Photo Credit
Uunganishwaji wa waya kwa ajili ya nishati ya umeme mjini Nairobi, Kenya(Picha ya World bank/video capture)