Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbadala wa kuni na mkaa utamrahisishia kazi mwanamke na kulinda misitu:Buhero

Mbadala wa kuni na mkaa utamrahisishia kazi mwanamke na kulinda misitu:Buhero

Pakua

Matumizi ya nishati haribifu kwa misitu na mazingira kama kuni na mkaa kwa kiasi kikubwa yakimuhusisha mwanamke yanahitaji nishati mbadala na hususani kwa nchi zinazoendelea ambako asilimia kubwa ya watu wanaishi vijijini na hawana fursa ya kupata nishati nyingine kwa matumizi ya kawaida. Serikali ya Tanzania imetambua hilo na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali likiwemo shirika la umoja wa Mataifa la mazingira UNEP na makampuni binafsi wanaihamasisha jamii kuingia katika matumizi ya gesi.

Hata hivyo kuna changamoto kubwa kufanikisha hilo , je serikali inalishughulikia vipi suala hilo sio tu kwa kumrahisishia kazi ya kusenya kuni mwanamke bali pia kulinda mazingira. Ungana na Flora Nducha na Bi Amina Akida Buhero afisa misitu wa wakala wa huduma za misitu Tanzani walio chini ya wizara ya maliasili na utalii anatoa jibu

 

Audio Credit
Siraj Kalyango/ Flora Nducha/ Amina Akida Buhero
Audio Duration
4'16"
Photo Credit
Mkaa, nishati ambayo inatumiwa na wengi lakini madhara yake kwa mazingira ni makubwa. (Picha:UN /Stuart Price)