Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya tumbaku yamepungua lakini bado kuna hatari- WHO

Matumizi ya tumbaku yamepungua lakini bado kuna hatari- WHO

Pakua

Kupitia ripoti yake iliyotolewa leo, WHO inasema matumizi hayo yamepungua kutoka asilimia 27 mwaka 2000 hadi asilimia 20 mwaka 2015.Mathalani idadi ya wanaume wenye umri wa miaka 15 wanaotumia tumbaku imepungua kutoka asilimia 43 mwaka 2000 hadi asilimia 34 mwaka 2015.

Halikadhalika kwa wanawake ni kutoka asilimia 11 mwaka 2000 hadi asilimia 6 mwaka 2015.

Hata hivyo WHO inasema kupungua huko hakutoshelezi kufikia lengo linalotakiwa la kuepusha watumiaji wa tumbaku kupata magonjwa ya moyo na magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza.

WHO inasema bado kuna tishio kwa kuwa watu wengi hawafahamu uhusiano kati ya kuvuta tumbaku na magonjwa ya moyo.

Mfano nchini China, utafiti uliofanyika umebaini kuwa asilimia 60 ya idadi ya watu nchini humo hawafahamu iwapo matumizi ya tumbaku husababisha magonjwa ya moyo.

Mkurugenzi wa WHO anayehusika na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs Dkt Douglas Bettcher, anafafanua..

(Sauti ya Dkt. Douglas Bettcher)

“Kuna vyote - tisho na matumaini. Ili kuona matumaini, inafaa kuweka masharti. Wakati tukichambua ripoti hii  tunakiri kuwa vifaa vinavyoitwa ‘N’,  vinasumu ndogo kuliko bidhaa za tumbaku asilia .Hatuwezi kuhakikisha kama  ni chombo muafaka kwa kuacha kabisa. Na pia tunaogopa kuwa watoto wana weza wakashawishika na kuanza kutumia vyote viwili.”

Hata hivyo amesema

(Sauti ya Dkt. Douglas Bettcher)

“Kiwango cha athari za afya ya binadamu itokanayo na matumizi ya tumbaku kinatisha. . Lakini habari njema ni kuwa vifo vingi vinavyotokana na matumizi yatumbaku vinazuilika  na tunaelewa fika kipi cha kufanya.”

Zaidi ya watu milioni 17.9 hufariki dunia kila mwaka kutokana na matumizi ya tumbaku.

 

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
2'19"
Photo Credit
WHO