Katu sitaki kurejea DRC, naogopa vita- Kijana mkimbizi

30 Mei 2018

Mchango wa vijana katika masuala mbalimbali ni dhahiri ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Hata hivyo mapigano na vita katika baadhi ya nchi ikiwemo Afrika imesababisha vijana kukimbia nchi zao na kusaka hifadhi nchi jirani.  Wengine sasa hata hawataki kurejea nyumbani na mchango wao uko mashakani.

Katika kuangazia mchango wa vijana katika jamii tunaelekea kambi ya Kyangwali huko Hoima nchini Uganda ambapo John Kibego amezungumza na vijana wakimbizi kuhusu utumikishaji na ukatili dhidi ya watoto na vijana.

 

Audio Credit:
John Kibego
Audio Duration:
3'10"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud