Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki wa kizazi kipya ndio unauza siku hizi.

Muziki wa kizazi kipya ndio unauza siku hizi.

Pakua

Muziki ni kifaa muhimu kinacholeta mabadiliko katika jamii.Muziki unaweza ukawafikia mamilioni ya watu,na kwa kuhamasisha jamii kuhusu changamoto za kijamii, kiuchumi na kimazingira ambavyo ndivyo msingi wa maendeleo endelevu SDGs.

Muziki unaendelea kuwa chanzo cha ajira pamoja na kiuchumi.Lakini muziki wenyewe hauwezi kuwa kifaa muhimu bila ya mchango wa mwanadamu , yaani mtunzi, muimbaji, mpiga ala na kazi nyingi nyinginezo. Kutokana na hayo makala ya leo yanamulika mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansa nchini Uganda.Kama wanavyosema kuishi kwingi ni kuona mengi. Na mmoja wa wanamuziki waliodumu muda mrefu nchini Uganda ni Moses Matovu, muasisi wa bendi ya AFRIGO ambayo nayo ndiyo bendi nzee kulikozote nchini humo. Kwa wengi MOSES MATOVU ndie msingi thabiti wa burudani kutoka kwa wanamuziki na vijana wengi chipukizi –kimuziki –wamelelewa nae.Ungana na Siraj Kalyango akikuletea mwanamuziki huyo.

......................................................

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
5'41"
Photo Credit
Picha: UM/Video capture